Zechariah 6:2-7

2 aGari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 3 bla tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 4 cNikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”

5 dMalaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6 eGari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”

7 fWakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

Copyright information for SwhKC